{"product_id":"kolonia-santita-laana-ya-panthera-tigrisi-9781477222959","title":"Kolonia Santita: Laana YA Panthera Tigrisi","description":"'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi - na duniani kwa jumla. \u003cbr\u003e Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda - na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili - na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.\u003cbr\u003e\u003cbr\u003e\u003cb\u003eAuthor:\u003c\/b\u003e Enock Maregesi\u003cbr\u003e\u003cb\u003ePublisher:\u003c\/b\u003e Authorhouse UK\u003cbr\u003e\u003cb\u003ePublished:\u003c\/b\u003e 09\/12\/2012\u003cbr\u003e\u003cb\u003ePages:\u003c\/b\u003e 406\u003cbr\u003e\u003cb\u003eBinding Type:\u003c\/b\u003e Paperback\u003cbr\u003e\u003cb\u003eWeight:\u003c\/b\u003e 1.31lbs\u003cbr\u003e\u003cb\u003eSize:\u003c\/b\u003e 9.00h x 6.00w x 0.90d\u003cbr\u003e\u003cb\u003eISBN:\u003c\/b\u003e 9781477222959\u003cbr\u003e\u003cb\u003eLanguage:\u003c\/b\u003e Swahili\u003cp\u003e\u003ci\u003eThis title is not returnable\u003c\/i\u003e\u003cbr\u003e\u003c\/p\u003e","brand":"Authorhouse UK","offers":[{"title":"Paperback","offer_id":45146180092019,"sku":"9781477222959","price":34.95,"currency_code":"EUR","in_stock":true}],"thumbnail_url":"\/\/cdn.shopify.com\/s\/files\/1\/0555\/9255\/0515\/files\/img_34ad6493-71f5-4d6d-a970-ef786b8d3eeb.jpg?v=1782925556","url":"https:\/\/bookstorenmore.com\/en-de\/products\/kolonia-santita-laana-ya-panthera-tigrisi-9781477222959","provider":"Bookstore N More","version":"1.0","type":"link"}